DIAMOND NA WEMA SEPETU SASA WATANGAZA NDOA!!
Huku mchumba’ke, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akifungasha
virago kurejea kwao, mzee mzima Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ ametangaza kumuoa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Awali kabla ya kufikia eneo la kutangaza kuoana, Diamond
aliweka wazi jukwaani kwamba yeye na Wema wamerudiana.
Baada ya shoo hiyo iliyomalizika saa moja usiku, paparazi
wetu alimfuata Diamond akiwa amesimama na Wema na kuwauliza kama
kweli wana nia ya kufunga ndoa. “Hilo mwana mbona lipo wazi, nataka
kumuoa staa na nataka kuzaa na staa,” alisema Diamond huku Wema
akiwa hapingi.


No comments:
Post a Comment