NGUMI:MAMLUKI NA WAFUASI WA CHADEMA NA ZITTO WACHAPANA MAKONDE NJE YA MAHAKAMA

Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wanaounga mkono uongozi wa juu
, jana walitwangana tena muda mfupi baada ya kuondoka eneo la
Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea huku Mahakama hiyo ikiahirisha hadi leo,
kutoa uamuzi wa maombi ya Zitto kuzuia kujadiliwa na Kamati Kuu ya Chadema.
Katika maombi hayo namba 1 ya mwaka 2014, Zitto ambaye pia ni
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, anaiomba Mahakama iizuie Kamati Kuu ya
Chadema kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake
hadi kesi yake ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Uamuzi wa maombi hayo ulipangwa kutolewa jana na Jaji John Utamwa
ambaye hata hivyo, alisema alikuwa hajamaliza kuandika uamuzi huo
na kuahirisha shauri hilo hadi leo mchana.
Maombi hayo ya Zitto ya zuio la muda la kujadiliwa na kuchukuliwa
uamuzi wowote kuhusu uanachama wake yametokana na kesi ya msingi
aliyoifungua mahakamani hapo Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wa
dhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Katika kesi hiyo, Zitto pia anaiomba Mahakama Kuu imwamuru Katibu Mkuu wa
Chadema ampatie mwenendo na taarifa za kikao cha Kamati Kuu za kumvua nyadhifa
zake zote alizokuwa nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika
utekelezaji wa majukumu yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini.
Mapigano
Baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, wanachama wa makundi yote
waliondoka eneo la Mahakama wakiendelea kuimba na kushangilia lakini walipofika eneo
la Mahakama ya Rufani ghafla walianza kupigana ngumi na mawe. Baadhi yao walikamatwa na askari kutokana na vurugu hizo.
Awali, wafuasi hao walifika mapema asubuhi katika viwanja vya
Mahakama tayari kusikiliza uamuzi huo.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa na askari polisi wakiwamo wale wa Kikosi
cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa na silaha pamoja na mabomu ya machozi walikuwa wametanda.
Pia kulikuwa na askari wa Kikosi cha Mbwa pamoja na gari la maji ya kuwasha.
Licha ya kuwahi, ni wafuasi wachache walioruhusiwa kuingia ndani
ya u`kumbi wa Mahakama tena baada ya kuandikisha majina yao huku w
No comments:
Post a Comment