
Wafunga ndoa hadharani wakiwa uchi wa mnyama huko Marekani, waenda kuilia honeymoon lupango.
Picha: wafunga ndoa hadharani wakiwa uchi wa mnyama huko Marekani, waenda kuilia honeymoon lupango
Dunia haiishi mambo na vijimambo, bibi na bwana harusi waliojikita katika kutetea haki za kupiga
picha uchi, Gypsy Taub na mkewe Jaymz Smith waishio San Francisco wamejikuta wakilia honeymoon yao
lupango baada ya kuchojoa nguo zao zote wakati wakifunga ndoa.
Kwa mujibu wa ‘The San Francisco Chronicle, bibi harusi alifika katika eneo la tukio akiwa amevaa nguo
kama kawaida lakini alizichojoa zote ghafla na kubaki mtupu kama alivyozaliwa kisha akapaza sauti, “hii
ni kwa ajili ya kupinga sheria zanazokataza kuwa mtupu kwa namna ambayo imekuwa katika ndoa.”
Naye mfungishaji ndoa ambaye sio kiongozi wa dini yeyote, alisema “najua watu wa San Francisco wako nyuma
yangu,” na kisha kuwaambia wana ndoa hao, “sasa mnaweza ku-kiss na kufanya ngono.”
Gazeti hilo limeripoti kuwa tukio hilo lilifanyika hadharani karibu na makazi ya watu ambapo wanawake wengi
na watoto walikuwa wakipita eneo hilo.
Baada ya shangwe za ndoa hiyo, maharusi walichukuliwa na gari la polisi na kupelekwa panapohusika, na ripoti
zinasema walifunguliwa mashitaka kwa kosa la kujiachia watupu hadharani.
Hata hivyo wawili hao waliachiwa baadae huku tarehe za honeymoon zikiwa zimeishia selo.
Lakini waliporudi uraiani waliliambia The San Francisco Chronicle kuwa ndoa yao ilikuwa nzuri na ya kufurahisha.
“It was fantastic…it surpassed all my expectations. It
No comments:
Post a Comment