Monday, December 30, 2013

HUDDAH MONROE WA KENYA AMPIGA DOGO JACK CLIFF KWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

HUDDAH MONROE WA KENYA AMPIGA DOGO JACK CLIFF KWA
 KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA
Aliyekuwa muwakilishi wa Kenya kwenye shindano
 la Big Brother Africa ‘The Chase’, Huddah Monroe
aka Thee Boss Lady amerusha dongo kwa mrembo wa Tanzania
 Jackie Cliff ambaye alikamatwa na dawa za kulevya aina ya Heroin nchini china.

Tweet ya Huddah inadai kuwa Jackie Cliff ni mrembo ambaye
 alitaka kuishi maisha mazuri ya haraka na kutumia vitu vya
 kifahari, pia akaambatanisha na picha mbili zinazomuonesha
Jackie akiwa amepozi kabla ya kukamatwa na nyingine akiwa na
pingu, picha iliyotolewa na gazeti la nchini China.

Katika tweet nyingine Huddah ambaye hupenda kuonesha maisha
 ya kifahari anayoishi,  amefunguka zaidi na kuonesha kuwa yeye
 ni muoga na asingeweza kufikia kiwango hicho.

“So this beautiful Tanzanian girl was caught with a KG of Cocaine.
 That’s now a BAD ASS B**CH! I’m such a coward…I swear I’m not BAD!” Huddah ametweet.




No comments:

Post a Comment